Sunday, September 9, 2018
NAMNA YA KUPIKA KEKI
Monday, September 3, 2018
MAPIGANO YAZUKA MJI MKUU WA LIBYA
Serikali ya Libya imetangaza hali ya hatari mara baada ya kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli na maeneo yaliyo karibu na mji huo, ambapo watu zaidi ya 39 wamefariki na wengine kujeruhiwa. Libya imetangaza hali hiyo ili kuweza kuwalinda raia wake, mali pamoja na asasi muhimu kwa jamii nzima na wageni wanaoingia nchini humo. Aidha, Serikali hiyo ya Libya imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha uhasama. Hata hivyo, wakati yakitokea hayo, takriban wafungwa 400 wametoroka kutoka gereza moja kusini mwa Tripoli, eneo ambalo pia limeshuhudia mapigano makali katika kipindi cha wiki moja kati ya makundi hasimu.
Friday, August 31, 2018
KUNDI LA PAKA LATIKISA LINDI
Kundi la paka wapatao 12 wameshiriki mazishi ya Salehe Matiko aliyezikwa saa 10 alasiri ya Agosti 24 katika Kijiji cha Chikalala mkoani Lindi. Marehemu Matiko aliuawa kwa kushambuliwa na wakazi wa kijiji hicho kwa tuhuma za ushirikina huku akidaiwa kuwatesa watu ikiwa ni pamoja na kuua ndugu zake. Wananchi wa kijiji hicho walieleza kuchoshwa na kile walichokiita mateso ya Matiko na kuamua kumuwinda na kumshambulia mpaka kupoteza maisha yake. Wakiwa msibani baada ya taratibu zote za kuandaa safari yake ya mwisho, jeneza lake lilibebwa kwa utaratibu wa kawaida lakini ghafla wakiwa barabarani kuelekea makaburini liliibuka kundi la paka lililokuwa likifuata jeneza hilo kwa nyuma hali iliyoibua hofu kwa wanakijiji. Lakini paka hao walifika hadi makaburini ambapo nao walishiriki mazishi yake. Wakati wa kushusha maiti kwenye kaburi lake, paka hao waliinamisha vichwa chini wakionesha utii wao kwa marehemu jambo ambalo liliwashtua wengi. Baada ya kumaliza taratibu zote za kumuhifadhi Matiko watu walioshiriki mazishi hao walitawanyika kama ilivyo ada lakini paka hao hawakutawanyika na badala yake waliendelea kubaki makaburini hapo. Msafiri Msemwa ambaye ni mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa, waliingia hofu kidogo kwa kuwa sio tukio la kawaida lakini waliendelea na taratibu za mazishi hayo. “Sio jambo la kawaida kutokea ndio maana kila mmoja alikuwa na hofu lakini watu waliendelea kama kawaida mpaka mwisho. “Kila mmoja alikuwa na tafsiri yake kutokana na kundi hilo la paka ambapo muda wote wa mazishi watu walikuwa wakiwatolea macho paka hao huku wakichukua tahadhari kwa lolote ambalo lingeweza kutokea,” amesema
Thursday, August 23, 2018
PILATO NI NANI?
Saturday, August 11, 2018
KITU CHA KWANZA ALICHOKISEMA RICH MAVOKO BAADA YA KUSHINDA KESI DHIDI YA WBC
Friday, August 10, 2018
MAHAKAMA YAAMURU KUONDOLEWA ZACHARIA NA LAUWO KATIKA KESI INAYOMKABIRI ALIYEKUWA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA SC
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu au kuifuta kesi hiyo. Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hans Poppe na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo. Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema bado wanaifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu lakini itafika mahali uvumilivu utawashinda na kama jamhuri wameshindwa basi waifute. Mahakama imeamuru Zacharia Hans Poppe (kulia) aondolewe kwenye kesi ya viongozi wa Simba SC “Ukiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” amesema Hakimu Simba. Awali, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na tayari wameshaifanyia marekebisho hati ya mashtaka na kwamba wanasubiri kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kesi hiyo iendelee kwa mujibu wa sheria. Baada ya Wakili huyo kudai hayo, Aveva aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibu za kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa imechukua muda mrefu huku Wakili wa Jamhuri Shadrack Kimaro na Wakili Takukuru, wamekuwa wakirushiana mpira. Kwa upande wake Kaburu ambaye ni mshtakiwa wa pili amedai kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita wako mahabusu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo huku mawakili hao wakidai faili liko kwa DPP. Alidai mshtakiwa wa kwanza, Aveva ana matatizo ya kiafya na kwamba kila wiki anaenda kliniki kwa ajili ya matibabu hivyo basi kuendelea kurushiana mpira ni kuwaumiza na kwamba hadhani kama DPP ameshindwa kushughulikia kesi yao, bali ni ucheweshaji wa makusudi unaofanywa na mawakili hao katika kesi hiyo kutoka kwa DPP na Takukuru. Amedai upelelezi umeshakamilika kilichobaki ni kubadilisha hati hiyo ili kesi ianze kusikilizwa, hivyo basi anaiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibuni ili waweze kuwaona na kuwaonea huruma kuliko kupanga tarehe za mbali za wiki mbili. Wakili Swai alidai kuwa, hoja zilizotolewa na washtakiwa hao zina mashiko na kuahidi kushughulikia suala hilo. Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo had I Agosti 17 mwaka huu. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli. Wanadaiwa, kuwa Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.
Monday, August 6, 2018
MDHAMINI MPYA SIMBA SC KUJENGA UWANJA WA BUNJU
SIMBA SC IMETAMBULISHA JEZI MPYA
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wametambulisha jezi zao mpya zitakazotumia msimu wa 2018/19. Kwamujibu wa Mkuu wa habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kuwa jezi hizo zitaanza kuuzwa rasmi hapo kesho kuanzia majira ya saa 10: 00 alasiri. Simba wamezitangaza jezi hizo ambazo zitatumika kwenye michezo mbalimballi. Wakati jezi zao nyeupe zitakuwa kwaajili ya mechi za ugenini huku nyekundu zikitumika kwa mechi za ugenini. Simba imetambulisha jezi hizo zenye nembo ya mdhamini mkuu SportPesa na Mo Energy Drink ambao ni wadhamini wapya waliotangazwa leo kwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 250.
Friday, August 3, 2018
UFAFANUZI WA TFF JUU YA ALIKIBA
Wednesday, August 1, 2018
ALIKIBA KUIKOSA MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ Ali Kiba amedaiwa anaweza akakosa mechi muhimu kabisa ndani ya Coastal Union. Ali Kiba ambaye alitangazwa kusajiliwa na timu hiyo ya mkoani Tanga wiki iliyopita, anasemekana kuwa ana aweza akakosa mechi yake ya kwanza ndani ya timu hiyo kutokana na shoo yake ya muziki. Ligi Kuu imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22 lakini ratiba ya shoo ya Alikiba inaonyesha itaanza Agosti 17, 18 na 25, mwaka huu huko Toronto, nchini Canada katika shoo iliyopewa jina la The All Star Music. Ratiba inaonyesha Coastal Union wataanza ligi, Agosti 22 dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hivyo Alikiba hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi hiyo. Meneja wa Coastal Union, Said Hilal ameweka wazi kuwa wanatambua majukumu ya kimuziki ya Ali Kiba hivyo hawana tatizo juu ya kukosa kwake mechi. Tunajua AliKiba ana majukumu yake mengi na sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kwenye hilo pale ambapo atakuwepo atafanya kazi na wenzake hivyo hakuna tatizo”.
Tuesday, July 31, 2018
TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO
Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 31.7.2018 Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri wa miaka 29, na wanaemtaka tu ni mlinda lango wa Ubelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, kutoka the Blues. (marca) Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Willian anasema ni mwenye ”furaha sana katika Chelsea na anafurahia kuishi London. (Globo Esporte, via Mirror) Meneja wa Leicester Claude Puel amesisitizia tena imani yake kwamba mlinzi wa England Harry Maguire mwenye umri wa miaka 25 – anayechezea Manchester United – atasalia na the Foxes katika msimu mpya. (Sky Sports) Maguire anatarajiwa kupewa donge nono katika mkataba wake mpya na Leicester na hivyo kuongezewa malipo yake ya wiki kutoka £50,000 hadi £95,000. (Mirror) Everton wako mstari wa mbele katika harakati za kusaini mkataba na Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester United na Argentina Marcos Rojo, mwenye umri wa miaka 28 ambae aliambiwa anaweza kuondoka kama tahamani yake ya £30m itatimizwa. (Mirror) Liverpool wanajiamini kuwa wao ndio watakao saini mkataba na mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, mwenye umri wa miaka 26, kwa mkataba wa muda mrefu mnamo wiki zijazo. (Mirror) Wakati huo huo , mchezaji wa the Reds kutoka Ubelgiji Divock Origi, 23, anasakwa kwa deni na Besiktas pamoja na Fenerbahce.(Talksport) The Blues wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey Chelsea wamekuwa na mazungumzo ya wazi na Inter Milan juu ya mchezaji wao wa safu ya kati , raia wa Uruguay Matias Vecino, mwenye umri wa miaka 26, na wakatoa £35.5m kwa Juventus ili wamchukue Muitaliano Mattia Caldara mwenye umri wa miaka anayecheza safu ya ulinzi katika timu ya taifa ya Italia. (London Evening Standard) The Blues pia wanaangalia uwezekano wa Kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal kutoka Wales -Aaron Ramsey, mweney umri wa miaka 27 kwa £30m (Telegraph) Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anasema lengo lake kuu ni kumpata mshambuliaji wa Buyern Munich Robert Lewandowski, Lazio amembiwa na the Gunners kuwa lazima walipe £7m ikiwa wanataka kusaini mkatapa na mchezaji wa safu ya mashambulizi Muhispania Lucas Perez. (Talksport) Newcastle wana nia ya kumchukua Nicolas Tagliafico wa Ajax na mchezaji wa kimataifa wa Argentina , lakini gharama ya £8m na madai ya mchezaji huyo wa safu ya nyuma kushoto mwenye umri wa miaka 23 huenda yakawa zaidi ya bajeti iliyopo ya meneja wa Magpies Rafael Benitez. (Newcastle Chronicle) Yanga wafanya Maamuzi haya kwa Rostand Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemtaja mchezaji wa Bayern Munich na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 29, kuwa ndiye mchezaji anayemlenga zaidi kumnunua (Star) Brighton imekubali kumuuza mshambuliaji wa England Sam Baldock mwenye umri wa miaka 29- kwa Reading. (Argus) Mourinho amewasihi wachezaji kama Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard wapunguze mapumziko yao wawasaidie wachezaji kwenye timu zao wasio na uwezo Leicester itakubali malipo ya £18m kumnunua mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, lakini hatma ya siku zijazo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 haijaamliwa mpaka mwishoni mwa Agosti wakati msimu wa uhamisho utakapomalizi (Leicester Mercury) Meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amekataa kuingizwa kwenye taarifa za uvumi zinazokihusisha kilabu na uhamisho wa mchezaji wa Chelsea na ttimu ya Ufaransa wa safu ya kati N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 27. (Talksport) Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amewatolea wito wachezaji kama vile Paul Pogba, Romelu Lukaku na Jesse Lingard, wote wakiwa na umri wa miaka 25, kupunguza mapumziko yao ili kuwasaidia wachezaji katika timu zao wenye uwezo mdogo ambao wameshindwa kufanikiwa kucheza mchezo wa kuridhisha katika kipindi cha kabla ya msimu (Times – subscription required) Mchezaji wa England anayeichezea kikosi cha Middlesbrough cha vijana walio chini ya miaka 21 kwa sasa Patrick Bamford, mwenye umri wa miaka 24, yuko karibu kuhamia kwa mahasimu wao katika Ligi ya Championi Leeds United kwa gharama ya awali ya awali ya kanda ya £7m. (Guardian) Wakati huo huo , Boro wamekataa pendekezo la Wolves ambao ni wageni katika Premier League ya kumchukua winga wao Adama Traore mwenye umri wa miaka 22 . (Express & Star) Mchezaji wa kiungo cha kati wa Morocco Younes Belhanda, anayeichezea Crystal Palace, amemua kuwa hatahamia England na kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 anasisitiza kuwa anafurahia kuwa Galatasary Turkish. (Football.London) Mchezaji wa safu ya kati wa Paris St-Germain Mfaransa Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 23, anakaribia kusaini mkataba na Ligue 1 champions. (ESPN) Mlinzi wa Everton Matty Pennington analengwa na Leeds – ambako alikuwa katika msimu uliopita kwa deni na Wigan pia wanamtaka Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 23.. (Liverpool Echo) Kocha wa zamani wa walinda lango Kevin Hitchcock ameteuliwa kufanya kazi hiyo hiyo katika timu ya Super Ligi ya India ya Chennaiyin FC -akijiunga na meneja wa zamani wa Aston Villa John Gregory. (Birmingham Mail)
Sunday, July 29, 2018
NYOTA YA MBWANA SAMATTA YAZIDI KUNG'ARA
NAHODHA wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, amezidi kuziumiza vichwa baadhi ya timu kubwa barani Ulaya baada ya Borussia Dortmund, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu Bundesliga, kuihitaji saini yake. Tayari Levante inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ imeshaweka mezani Euro milioni 4 ili kuinasa saini ya Mtanzania huyo huku timu yake ya Genk ya Ubelgiji, ikisema kiasi hicho cha fedha ni kidogo kulinganisha na uwezo wa mchezaji wao. Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema Dortmund pamoja na Metz ya Ufaransa nazo zinaitaka huduma ya Samatta japo Levante ndio walioko kwenye kasi kubwa. “Licha ya kwamba Levante ndio wameenda rasmi lakini hata Borussia (Dortmund) na Metz, nao wameonyesha nia ya kuitaka saini yake, nadhani muda sio mrefu kila kitu kitakuwa wazi,” alisema. Kama Dortmund watafika bei inamaanisha Samatta atakwenda kugombania namba na akina Shinji Kagawa na Mario Gotze. Katika hatua nyingine Samatta leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Lokeren, mchezo wao wa ufunguzi Ligi Kuu nchini Ubelgiji. Msimu mpya wa ligi nchini humo umeanza juzi Ijumaa na Genk ya Samatta, wao wanaianza safari yao ya kuusaka ubingwa leo ugenini dhidi ya wapinzani wao hao Uwanja wa Daknamstadio. Baada ya mchezo huo wa ligi, kikosi hicho cha Genk kitakuwa na kazi nyingine Jumatano kucheza na Fola Esch mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Europa League. Genk wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kwani mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana katikati ya wiki hii, kikosi hicho cha akina Samatta kilishinda mabao 5-0 nyumbani
Friday, July 27, 2018
AHADI YA KOREA KASKAZINI KWA MAREKANI YAANZA KUTEKELEZWA
Korea Kaskazini yarejesha mabaki ya Wamarekani waliokufa vitani Korea Kaskazini yarejesha mabaki ya Wamarekani waliokufa vitani Korea Kaskazini imeanza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wao, Kim Jong-un kwa kurejesha mabaki ya wanajeshi wa Marekani waliokufa kwenye ardhi ya nchi hiyo. Nchi hiyo imeripotiwa kukabidhi kwa jeshi la Marekani mabaki ya maelfu ya waliokuwa wapiganaji wa Marekani waliokufa kwenye vita kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, mwaka 1950-1953. Ndege ya jeshi la Marekani imefanya safari kadhaa kwenye Pwani ya Korea Kaskazini na kubeba mabaki hayo ambayo yamepelekwa nchini Korea Kusini. Kim Jong-un alimuahidi Trump kuwa atakabidhi mabaki hayo walipokutana nchini Singapore; na hii imekuwa ahadi ya kwanza inayoonekana kutekelezwa kwa kiwango cha asilimia 100. Ikulu ya Marekani imeelezwa kufurahishwa na hatua hiyo ya Korea Kaskazini. “Leo Kim Jong-un ametekeleza sehemu ya ahadi yake aliyompa Rais Trump kurejesha mabaki ya wapiganaji wetu. Tumetiwa moyo na hatua iliyochukuliwa na Korea Kaskazini kwa ajili ya mabadiliko chanya,” imeeleza taarifa hiyo. Kwa mujibu wa ratiba, Agosti 1 mwaka huu wanajeshi wa Marekani watatoa heshima zao kwa mabaki ya wapiganaji hao katika eneo la kijeshi la Osan nchini Korea Kusini. Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 27, 2018 Takribani wanajeshi 7,700 wa Marekani wanatajwa kupoteza maisha kwenye vita ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, katika miaka ya 1950. Mabaki ya askari 5,300 wa Marekani yalikuwa kwenye ardhi ya Korea Kaskazini. Katika vita hiyo mbaya kuwahi kutokea kwenye eneo hilo, mamilioni ya watu walipoteza maisha ikiwa ni pamoja na wanajeshi 36,000 wa Marekani.
KUPATWA KWA MWEZI
Tuesday, July 24, 2018
TETESI ZA USAJILI COASTAL UNION
Saturday, July 21, 2018
THIS IS SIMBA
Usajili mwingine uliokamilika usiku wa Jana Simba huu hapa - July 21, 2018 . Usajili mwingine uliokamilika Ukisikia Simba hawatanii hawatanii kweli na wamekuwa tayari kufanya lolote linapokuja suala la Kumuhitaji mchezaji mzuri ambaye wanaamini anaweza Kuwasaidia kwenye Kikosi chao kwaajili ya ligi Kuu na mashindano mengine kitaifa na Kimataifa ambayo watashiriki. Simba siku ya Jana wamefanikiwa kumnasa Kiungo mzambia Chama Clatous kutoka katika Klabu ya Dynamos Fc ya Huko nchini Zambia.
Friday, July 20, 2018
WEMA SEPETU AACHIWA HURU
Wednesday, July 18, 2018
ZAIDI YA NUSU YA BIDHAA KATIKA SOKO LA NCHI YA UGANDA NI FEKI
Tuesday, July 17, 2018
WASTAAFU KULIPWA
MBAPE ATOA MSAADA FEDHA ZOTE ALIZOPATA KOMBE LA DUNIA
Kylian Mbappe atoa msaada fedha zote alizokusanya kombe la Dunia Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe ameonyesha moyo wa kipekee baada ya kutoa msaada fedha zote alizopata kwenye michinuano ya kombe la dunia dola 550,000 sawa na bilioni 1.2 za Kitanzania kwa kituo kinachotoa huduma ya michezo kwa watoto wenye ulemavu.Mbappe mwenye umri wa miaka 19 ametoa kiasi hicho cha dola za Kimarekani 550,000 ambazo zinatokana na posho pamoja na 'bonus' ya ushindi wa kombe la dunia mwaka huu 2018. Mchezaji huyo amefunga jumla ya mabao manne kwenye michuano hiyo akiitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa ametoa fedha hizo kwenye kituo cha Premiers de Cordee kinacho husika na kutoa bure huduma za michezo kwa watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama pamoja na wanamichezo watoto wenye ulemavu. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha L'Equipe kutoka nchini Ufaransa kimeeleza kuwa Mbappe hajabakiza hata kiasi kidogo cha fedha hiyo aliyopata kwenye kombe la dunia ambayo ni dola 22,500 kwa michezo iliyoshiriki timu ya Ufaransa na dola za Kimarekani 350,000 kama 'bonus' baada ya Les Bleus kushinda taji baada ya kuifunga Croatia jumla ya mabao 4 - 2.
MANENO YA RONALDO BAADA YA KUTUA JUVENTUS
Haya ndio maneno ya Ronaldo baada ya kutambulishwa Juventus Mchezaji mpya wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Crisstiano Ronaldo jana ameweza kutambulishwa rasmi katika klabu hiyo na kuchukuliwa vipimo vya kiafya.Baadhi ya kauli alizozitoa mshambuliaji huyo wakati anazungumza na waandishi zimetafsiriwa tofauti na wadau mbalimbali wa michezo. "Mimi ni tofauti na wachezaji wengine wote ambao wanafikiri kazi yao iko juu ya umri wangu," alisema Ronaldo. Aliongeza, "Ninataka kuonyesha kwamba mimi si kama wengine, mimi ni tofauti, ni wakati mzuri sana kwangu na klabu kwa sababu mimi sina miaka 23, bali nina miaka 33. Umri wangu sio tatizo sana najisikia vizuri sana,najisikia kuhamasika, na nina furaha,"Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kwa kitita cha Euro mil 100 amesema atajumuika kwenye mazoezi na wachezaji wenzake wa timu hiyo Julai 30 mwaka huu. Ronaldo amefanikiwa kufunga magoli 450 katika klabu ya Real Madrid kwa muda wa misimu 9 huku akiisaidia kutwaa mataji 15 mataji manne ya UEFA na mawili ya Laliga,huku akichukua tuzo ya mchezaji bora Duniani Ballon d or mara tano.
MREMBO WA KIRUSI ANASWA KWA KUNYAPIA NYAPIA MAMBO YA MAREKANI
Monday, July 16, 2018
RAIA INDONESIA WALIPA KISASI
Kundi la wanakijiji nchini Indonesia wamefanikiwa kuwaua mamba wapatao 300 kwenye makao makuu ya wanyama katika mkoa was West Papua.
Mauaji hayo yalikuwa ni yakulipiza kisasi cha kifo cha mwanaume mmoja aliyeuawa katika eneo hilo.
Maafisa wa polisi wanasema hawakuweza kuzuia mauaji hayo ila watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika katika mauaji hayo.
Kwa makosa kama haya nchini Indonesia adhabu yake ni pamoja na kifungo.
Wednesday, July 11, 2018
SIMBA SC YATINGA FINALI
Simba sc imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kagame Super Cup.Simba sc wamelazimika kusubiri hadi dakika ya (41) ambapo mchezaji mwenye asili ya kinyarwanda Meddie Kagere amefanikiwa kukwamisha mpira nyavuni.
Monday, July 9, 2018
HATUA MOJA HUANZISHA NYINGINE
Katibu mkuu kiongozi,John Kijazi amesema mpaka mwishoni mwa mwaka huu serikali itakuwa imeagiza ndege nyingine mbili aina ya Bombardier hivyo kufanya kuwa na ndege sita za kisasa.
"Mwito wangu kwa ATCL,watunze ndege hizi na kuhakikisha wanazihudumia vizuri na kuendesha kibiashara.kwa kufanya hivyo serikali itakuwa na uwezo wa kununua ndege nyingine."amesema
Tuesday, July 3, 2018
Tuesday, June 26, 2018
YAMETIMIA
Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Gor Mahia ya nchini Kenya.
Mshambuliaji huyu raia wa Rwanda amesajiliwa kwa kitita cha shilingi ml. 110.
DEAL DONE
Kiungo mbelgiji Radja Nainggolan aliyekuwa akikipiga katika klabu ya AS Roma amejiunga na klabu ya Inter Milan kwa Euro 21
Monday, June 25, 2018
PACHA WALIOUNGANA KUPELEKWA SAUDI ARABIA
Mfalme wa Saudi Arabia amekubali pacha walioungana,Marines na Anisia Beatus kupelekwa nchini humo kuangalia uwezekano wa kuwatenganisha mapacha hao walioungana sehemu ya kifuani.
Mapacha hao wamelazwa katika hospitali ya Muhimbili (MNH) tangu februari wakipatiwa matibabu.
Thursday, June 7, 2018
CHINI YA KAPETI
Klabu ya Singida United imetibitisha uwezekano mdogo wa kuikosa huduma ya mchezaji wake Deus Kaseke.
Kwa mujibu wa msemaji wake,Festo Sanga amesema,"Kuna uwezekano mdogo wa kupata huduma ya mchezaji huyo kutokana klabu moja ya Afrika kusini kuhitaji huduma yake".
MWENDELEZO WA SPORTPESA SUPER
KIKOSI CHA SIMBA VS KK HOMEBOYZ
1.Aishi Manula
2.Shomari Kapombe
3.Mohamed Zimbwe
4.Paul Bukaba
5.Erasto Nyoni
6.Jonasi Mkude
7.Shiza Kichuya
8.Muzamiru Yassin
9.Mohammed Rashid
10.Rashid Juma
11.Haruna Niyonzima
SUB.
1.Salim Ally
2.Ally Shomari
3.Yusufu Mlipili
4.Mohamed Ibrahim
5.Marcel Kaheza
6.Adamu Salamba
Wednesday, June 6, 2018
KAZI YA KUENEZA WOKOVU NA CHANGAMOTO ZAKE
Ethiopia
Mchungaji mmoja kwa Majina Docho Eshete ameuawa kwa kushambuliwa na mamba akiwa anawafanyia ubatizo waumini wapya ziwani
Habari mpya
Ajali mbaya imetokea mkoani Kigoma Kahabwa Kata ya Gungu.
Ajali hiyo imehusisha treni ya mizigo name basi lifanyalo safari za Kigoma -Tabora
MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI
Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...
-
Pontio Pilato Alikuwa Nani? “PILATO alikuwa mtu mwenye dhihaka, mwenye kutilia shaka mambo, na anayewashangaza watu. Watu fulani humwona ku...
-
NAMNA YA KUPIKA KEKI MAHITAJI: -Mayai sita -Siagi -Sukari (icing sugar) -Baking powder -Unga wa ngano -Mafuta ya kupikia -Flavours za vanill...
-
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wametambulisha jezi zao mpya zitakazotumia msimu wa 2018/19. Kwamujibu wa Mkuu wa habari na...