Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ Ali Kiba amedaiwa anaweza akakosa mechi muhimu kabisa ndani ya Coastal Union. Ali Kiba ambaye alitangazwa kusajiliwa na timu hiyo ya mkoani Tanga wiki iliyopita, anasemekana kuwa ana aweza akakosa mechi yake ya kwanza ndani ya timu hiyo kutokana na shoo yake ya muziki. Ligi Kuu imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22 lakini ratiba ya shoo ya Alikiba inaonyesha itaanza Agosti 17, 18 na 25, mwaka huu huko Toronto, nchini Canada katika shoo iliyopewa jina la The All Star Music. Ratiba inaonyesha Coastal Union wataanza ligi, Agosti 22 dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hivyo Alikiba hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi hiyo. Meneja wa Coastal Union, Said Hilal ameweka wazi kuwa wanatambua majukumu ya kimuziki ya Ali Kiba hivyo hawana tatizo juu ya kukosa kwake mechi. Tunajua AliKiba ana majukumu yake mengi na sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kwenye hilo pale ambapo atakuwepo atafanya kazi na wenzake hivyo hakuna tatizo”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI
Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...
-
Pontio Pilato Alikuwa Nani? “PILATO alikuwa mtu mwenye dhihaka, mwenye kutilia shaka mambo, na anayewashangaza watu. Watu fulani humwona ku...
-
NAMNA YA KUPIKA KEKI MAHITAJI: -Mayai sita -Siagi -Sukari (icing sugar) -Baking powder -Unga wa ngano -Mafuta ya kupikia -Flavours za vanill...
-
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wametambulisha jezi zao mpya zitakazotumia msimu wa 2018/19. Kwamujibu wa Mkuu wa habari na...
No comments:
Post a Comment