Friday, July 27, 2018
KUPATWA KWA MWEZI


Leo usiku Watanzania kushuhudia tukio refu zaidi la kupatwa kwa mwezi katika historia, Kama umefanikiwa kuiona Ijumaa ya leo Julai 27, 2018 basi mshukuru Mungu sana kwani umepata bahati ya kushuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa mwezi usiku wa leo.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwenye Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) tukio hilo litatokea majira ya kuanzia saa 4:30 usiku hadi 6:14 .
Tukio la kupatwa kwa mwezi linatarajiwa kuonekana vizuri katika maeneo mengi ya bara la Afrika, Asia na Ulaya. Hapa nchini Tanzania tukio hilo linatarajiwa kuonekana katika maeneo mengi na linatarajiwa kudumu kwa takribani masaa mawili.
Kupatwa kwa Mwezi hutokea wakati Dunia, Mwezi na Jua vinapokuwa kwenye mstari mmoja. Hali hiyo inapotokea mwanga wa jua unaofika katika uso wa mwezi huzuiwa na duara la Dunia. Katika mpangilio huo nuru ya Mwezi huonekana kuwa na giza (Total Lunar Eclipse), hali inayotarajiwa kujitokeza katika maeneo ya bara la Afrika, Asia na Ulaya usiku wa leo tarehe 27 Julai 2018.
Kupatwa kwa Mwezi husababisha mabadiliko katika nuru ya mwezi na hivyo kufanya nuru ya mwezi kuwa hafifu(Partial Lunar Eclipse) au kuwa giza (Total Lunar Eclipse). Kwa kuwa kupatwa kwa mwezi kutatokea kipindi Mwezi ukiwa mbali zaidi na Dunia, inatarajiwa kuwa tukio hili litaonekana kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na matukio mengine katika karne ya 21.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI
Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...
-
Pontio Pilato Alikuwa Nani? “PILATO alikuwa mtu mwenye dhihaka, mwenye kutilia shaka mambo, na anayewashangaza watu. Watu fulani humwona ku...
-
Tetesi za Usajili barani Ulaya leo 31.7.2018 Real Madrid haina mpango wa kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Willian, mwenye umri ...
-
NAMNA YA KUPIKA KEKI MAHITAJI: -Mayai sita -Siagi -Sukari (icing sugar) -Baking powder -Unga wa ngano -Mafuta ya kupikia -Flavours za vanill...
No comments:
Post a Comment