Tuesday, July 17, 2018

WASTAAFU KULIPWA

 MENU NYUMBANI HABARI BURUDANI MICHEZO SIASA ZETU MAGAZETI ZAIDI  HABARI Wastaafu kabla ya 1999 kuanza kulipwa 1 min ago Comments Off on Wastaafu kabla ya 1999 kuanza kulipwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali inaendelea kufanya uchambuzi wa kubaini watumishi wote waliostaafu kabla ya 1999 ambao walikuwa wakichangia katika mifuko ya hifadhi ya Jamii ili waweze kulipwa madai yao ambapo mpaka sasa ni shilingi Bilioni 150 zimeshalipwa. Akizungumza na watumishi wa Chama cha Walimu Tanzania CWT kwa niaba ya Waziri Mhagama, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge kazi ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema ni dhamara ya Serikali kuhakikisha wastaafu wote wakiwemo walimu wanalipwa madai yao. Kwa upande wake Rais wa Chama cha Walimu Tanzania CWT, Leah Ulaya amesema changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo ni baadhi ya vyama vinavyopingana na CWT kuleta mgogoro ndani ya chama hali inayofanya wanachama kushindwa kupata haki zao. Video: Nape aitega Serikali, CCM yaandika historia mpya Video: Rais Magufuli afungua Mkutano wa Dunia wa Vyama vya Siasa Naye katibu Mkuu wa CWT Taifa Mwalimu Deus Seif amesema kuwa walimu wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali ambazo zinapelekea baadhi ya walimu kutotekeleza majukumu yao vyema. Hivyo wameiomba Serikali kuipa kipaumbele kada hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

No comments:

Post a Comment

MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...