Sunday, September 9, 2018

NAMNA YA KUPIKA KEKI

NAMNA YA KUPIKA KEKI MAHITAJI: -Mayai sita -Siagi -Sukari (icing sugar) -Baking powder -Unga wa ngano -Mafuta ya kupikia -Flavours za vanilla, choklate au matunda NAMNA YA KUANDAA Chukua mayai yako sita (kwa keki ya ukubwa wa wastani), yagonge kisha chukua siagi (robo kilo) na uiweke kwenye bakuli, ongeza na sukari kwenye siagi kisha mimina mayai kwenye mchanganyiko huo. Koroga mpaka upate uji mzito, unaweza kutumia mashine maalum ya kuchanganyia. Ukishapata uji mzito lakini laini, changanya na unga wa ngano, ongeza baking powder kijiko cha chai kisha weka flavour yoyote unayotaka keki yako iwe, inaweza kuwa vanilla, rose, machungwa, mananasi n.k. Changanya mchanganyiko huo kwa kutumia mwiko kwa dakika mbili mfululizo. Chukua sufuria, ipake mafuta kwa ndani kisha chukua karatasi plain na kuiweka ndani ya sufuria. Mwagia mchanganyiko wako kisha weka kwenye oven na baada ya muda utaanza kusikia harufu nzuri. Ukitaka kujua kama keki yako imeiva, chukua kijiti kikavu na kukiingiza katikati ya keki, kikitoka kikavu basi ujue keki yako imeiva, itoe na iache ipoe, unaweza kuongeza na mapambo unayoyataka, kama kuandika jina au kuweka rangi.

Monday, September 3, 2018

MAPIGANO YAZUKA MJI MKUU WA LIBYA

Serikali ya Libya imetangaza hali ya hatari mara baada ya kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli na maeneo yaliyo karibu na mji huo, ambapo watu zaidi ya 39 wamefariki na wengine kujeruhiwa. Libya imetangaza hali hiyo ili kuweza kuwalinda raia wake, mali pamoja na asasi muhimu kwa jamii nzima na wageni wanaoingia nchini humo. Aidha, Serikali hiyo ya Libya imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha uhasama. Hata hivyo, wakati yakitokea hayo, takriban wafungwa 400 wametoroka kutoka gereza moja kusini mwa Tripoli, eneo ambalo pia limeshuhudia mapigano makali katika kipindi cha wiki moja kati ya makundi hasimu.

MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...