Wednesday, March 6, 2019

MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taifa hilo aliyekuwa akiugua na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi, HIV hana tena virusi hivyo. Mgonjwa huyo ambaye pia amekuwa akiugua saratani amekuwa akifuatiliwa kwa kipindi cha miezi 18 sasa na kuabinika kwamba viini vinavyosababisha maradhi hayo havionekani tena katika mwili wake baada ya kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha hali hiyo kwa kuwekewa chembechembe zisizokuwa na maradhi. Watafiti hao wa Chuo cha University College London, Imperial College London, na vyuo vikuu vya Cambridge na Oxford hata hivyo wamesema bado ni mapema kutangaza rasmi kuwa mgonjwa huyo amepona kabisa. Mwanamume huyo alibainika kuugua ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2003. Kisa kingine cha mgonjwa kuripotiwa kupona ugonjwa huo, ilikuwa miaka takriban kumi iliyopita ,ambapo mgonjwa aliyefanyiwa bone marrow transpant alipona kabisa.

Sunday, September 9, 2018

NAMNA YA KUPIKA KEKI

NAMNA YA KUPIKA KEKI MAHITAJI: -Mayai sita -Siagi -Sukari (icing sugar) -Baking powder -Unga wa ngano -Mafuta ya kupikia -Flavours za vanilla, choklate au matunda NAMNA YA KUANDAA Chukua mayai yako sita (kwa keki ya ukubwa wa wastani), yagonge kisha chukua siagi (robo kilo) na uiweke kwenye bakuli, ongeza na sukari kwenye siagi kisha mimina mayai kwenye mchanganyiko huo. Koroga mpaka upate uji mzito, unaweza kutumia mashine maalum ya kuchanganyia. Ukishapata uji mzito lakini laini, changanya na unga wa ngano, ongeza baking powder kijiko cha chai kisha weka flavour yoyote unayotaka keki yako iwe, inaweza kuwa vanilla, rose, machungwa, mananasi n.k. Changanya mchanganyiko huo kwa kutumia mwiko kwa dakika mbili mfululizo. Chukua sufuria, ipake mafuta kwa ndani kisha chukua karatasi plain na kuiweka ndani ya sufuria. Mwagia mchanganyiko wako kisha weka kwenye oven na baada ya muda utaanza kusikia harufu nzuri. Ukitaka kujua kama keki yako imeiva, chukua kijiti kikavu na kukiingiza katikati ya keki, kikitoka kikavu basi ujue keki yako imeiva, itoe na iache ipoe, unaweza kuongeza na mapambo unayoyataka, kama kuandika jina au kuweka rangi.

Monday, September 3, 2018

MAPIGANO YAZUKA MJI MKUU WA LIBYA

Serikali ya Libya imetangaza hali ya hatari mara baada ya kuzuka kwa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli na maeneo yaliyo karibu na mji huo, ambapo watu zaidi ya 39 wamefariki na wengine kujeruhiwa. Libya imetangaza hali hiyo ili kuweza kuwalinda raia wake, mali pamoja na asasi muhimu kwa jamii nzima na wageni wanaoingia nchini humo. Aidha, Serikali hiyo ya Libya imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo na kuheshimiwa kwa makubaliano ya kusitisha uhasama. Hata hivyo, wakati yakitokea hayo, takriban wafungwa 400 wametoroka kutoka gereza moja kusini mwa Tripoli, eneo ambalo pia limeshuhudia mapigano makali katika kipindi cha wiki moja kati ya makundi hasimu.

Friday, August 31, 2018

KUNDI LA PAKA LATIKISA LINDI

Kundi la paka wapatao 12 wameshiriki mazishi ya Salehe Matiko aliyezikwa saa 10 alasiri ya Agosti 24 katika Kijiji cha Chikalala mkoani Lindi. Marehemu Matiko aliuawa kwa kushambuliwa na wakazi wa kijiji hicho kwa tuhuma za ushirikina huku akidaiwa kuwatesa watu ikiwa ni pamoja na kuua ndugu zake. Wananchi wa kijiji hicho walieleza kuchoshwa na kile walichokiita mateso ya Matiko na kuamua kumuwinda na kumshambulia mpaka kupoteza maisha yake. Wakiwa msibani baada ya taratibu zote za kuandaa safari yake ya mwisho, jeneza lake lilibebwa kwa utaratibu wa kawaida lakini ghafla wakiwa barabarani kuelekea makaburini liliibuka kundi la paka lililokuwa likifuata jeneza hilo kwa nyuma hali iliyoibua hofu kwa wanakijiji. Lakini paka hao walifika hadi makaburini ambapo nao walishiriki mazishi yake. Wakati wa kushusha maiti kwenye kaburi lake, paka hao waliinamisha vichwa chini wakionesha utii wao kwa marehemu jambo ambalo liliwashtua wengi. Baada ya kumaliza taratibu zote za kumuhifadhi Matiko watu walioshiriki mazishi hao walitawanyika kama ilivyo ada lakini paka hao hawakutawanyika na badala yake waliendelea kubaki makaburini hapo. Msafiri Msemwa ambaye ni mkazi wa kijiji hicho ameeleza kuwa, waliingia hofu kidogo kwa kuwa sio tukio la kawaida lakini waliendelea na taratibu za mazishi hayo. “Sio jambo la kawaida kutokea ndio maana kila mmoja alikuwa na hofu lakini watu waliendelea kama kawaida mpaka mwisho. “Kila mmoja alikuwa na tafsiri yake kutokana na kundi hilo la paka ambapo muda wote wa mazishi watu walikuwa wakiwatolea macho paka hao huku wakichukua tahadhari kwa lolote ambalo lingeweza kutokea,” amesema

Thursday, August 23, 2018

PILATO NI NANI?

Pontio Pilato Alikuwa Nani? “PILATO alikuwa mtu mwenye dhihaka, mwenye kutilia shaka mambo, na anayewashangaza watu. Watu fulani humwona kuwa mtakatifu, wengine humwona kuwa mtu dhaifu, mwanasiasa aliyekuwa tayari kumdhabihu mtu mmoja ili kuepuka mizozo.”—Pontius Pilate, kitabu kilichoandikwa na Ann Wroe. Uwe unakubaliana na maoni hayo au la, Pontio Pilato alijulikana sana kwa sababu ya jinsi alivyomtendea Yesu Kristo. Pilato alikuwa nani? Tunajua nini kumhusu? Kufahamu vizuri cheo chake kutatusaidia kuelewa matukio muhimu zaidi kuwahi kutukia duniani. Cheo, Kazi, na Mamlaka Maliki Mroma Tiberio alimtawaza Pilato kuwa gavana wa mkoa wa Yudea mwaka wa 26 W.K. Maliwali kama hao walikuwa wanajeshi wa kupanda farasi, yaani, walikuwa na cheo cha chini, wakilinganishwa na watu waliokuwa na vyeo vya juu serikalini. Yaelekea Pilato alijiunga na jeshi akiwa kamanda wa cheo cha chini; kisha akapandishwa cheo hatua kwa hatua; na hatimaye akawekwa rasmi kuwa gavana akiwa na umri usiozidi miaka 30. Pindi fulani, Pilato alivalia mavazi ya kijeshi, yaani, koti la ngozi na bamba la kifuani la chuma. Hadharani alivalia kanzu nyeupe yenye pindo za zambarau. Huenda alikuwa na nywele fupi na alinyoa ndevu zote. Ingawa watu fulani huamini kwamba alitoka Hispania, jina lake linaonyesha alikuwa wa kabila la Pontii, yaani, wakuu wa Wasamnite kutoka kusini mwa Italia. Kwa kawaida maliwali wa cheo cha Pilato walitumwa katika maeneo yasiyostaarabika. Waroma waliona Yudea kuwa mojawapo ya maeneo hayo. Mbali na kudumisha amani, Pilato alisimamia kodi zisizo za moja kwa moja na kodi ya kichwa. Kila siku mahakama za Wayahudi zilishughulikia udumishaji wa haki, lakini kesi zilizohitaji hukumu ya kifo zilipelekwa kwa gavana, ambaye alikuwa na mamlaka kuu zaidi ya kuhukumu. Pilato na mke wake pamoja na waandishi wachache, marafiki na wajumbe kadhaa, waliishi katika jiji la bandarini la Kaisaria. Pilato alisimamia vikosi vitano vya wanajeshi wa kwenda kwa miguu, kila kimoja kikiwa na watu 500 hadi 1,000 na pia wanajeshi 500 wanaopanda farasi. Kwa ukawaida askari wake waliwatundika watu waliovunja sheria. Kulipokuwa na amani, wakosaji waliuawa baada ya kesi kusikilizwa kwa muda mfupi, lakini kulipokuwa na ghasia, waasi waliuawa papo hapo wakiwa wengi. Kwa mfano, Waroma waliwatundika watumwa 6,000 ili kukomesha uasi ulioongozwa na Spartacus. Kulipokuwa na matatizo huko Yudea, kwa kawaida gavana aliwasiliana na mwakilishi wa maliki huko Siria ambaye alisimamia vikosi vya wanajeshi 3,000 hadi 6,000. Hata hivyo, kwa muda mwingi ambao Pilato alikuwa gavana, hakukuwa na mwakilishi huko Siria na hivyo Pilato alilazimika kukomesha ghasia upesi. Kwa kawaida, magavana waliwasiliana na maliki. Mambo yaliyohusu cheo chake au tisho lolote kuelekea utawala wa Roma lilipaswa kuripotiwa kwa maliki, kisha sheria za kifalme zingetungwa. Yaelekea gavana alijitahidi kumweleza maliki mambo yanayohusu mkoa wake kabla ya watu kulalamika. Matatizo yalipoanza huko Yudea, Pilato alikuwa na wasiwasi sana. Mbali na masimulizi ya Injili, wanahistoria Flavio Yosefo na Philo ndio walioandika mambo mengi kumhusu Pilato. Pia, mwanahistoria Mroma, Tasito alieleza kwamba Pilato alimuua Christus, ambaye Wakristo wanaitwa kwa jina lake. Hasira ya Wayahudi Yachochewa Yosefo anasema kwamba kwa sababu ya sheria ya Wayahudi iliyopinga kutengeneza sanamu, magavana Waroma hawakupeleka huko Yerusalemu bendera za kijeshi zilizokuwa na sanamu za maliki. Kwa kuwa Pilato hakuheshimu sheria hiyo, Wayahudi wenye hasira walipeleka malalamiko yao Kaisaria. Kwa siku tano, Pilato hakuchukua hatua yoyote. Siku ya sita, akawaamuru askari wake wawazingire walalamikaji na kutisha kuwaua iwapo hawatatawanyika. Wayahudi waliposema kwamba afadhali wafe kuliko kuona Sheria yao ikivunjwa, Pilato alitulia na kuamuru sanamu hizo ziondolewe. Pilato hakujizuia kutumia nguvu. Katika kisa kimoja kilichoandikwa na Yosefo, Pilato alianzisha mradi wa kutengeneza mfereji wa kuleta maji Yerusalemu na kuendeleza mradi huo kwa kutumia pesa za hazina ya hekalu. Pilato hakuchukua pesa hizo waziwazi, kwa kuwa alijua kwamba ni kukufuru kupora hekalu, na hilo lingewafanya Wayahudi wenye hasira wamwombe Tiberio amfute kazi. Hivyo, yaelekea Pilato alishirikiana na wasimamizi wa hekalu. Pesa zilizowekwa wakfu, zilizoitwa “korbani” zingeweza kutumiwa kihalali kufanya kazi ambazo zingewanufaisha wakaaji wa jiji. Lakini maelfu ya Wayahudi walikusanyika kuonyesha ghadhabu yao. Pilato aliwaagiza askari wachangamane na umati, naye akawaamuru wasitumie upanga bali wawapige walalamikaji kwa rungu. Yaelekea alitaka kuudhibiti umati bila kuchochea mauaji. Inaonekana alifaulu, ingawa watu kadhaa walikufa. Huenda watu waliomwambia Yesu kwamba Pilato alichanganya damu ya Wagalilaya na dhabihu zao walikuwa wakirejelea tukio hilo.—Luka 13:1. “Kweli Ni Nini?” Pilato alijulikana kwa sababu ya uchunguzi aliofanya kuhusu mashtaka ya makuhani wakuu Wayahudi na wanaume wazee yaliyosema kwamba Yesu alijifanya kuwa Mfalme. Aliposikia kwamba Yesu alikuja kutoa ushahidi kwa ajili ya ile kweli, Pilato aliona kwamba mfungwa huyo hakuwa tisho kwa Roma. “Kweli ni nini?” akauliza, akifikiri kwamba kweli ni wazo lisiloweza kueleweka na halihitaji kufikiriwa sana. Alikata kauli gani? “Mimi sioni uhalifu wa mtu huyu.”—Yohana 18:37, 38; Luka 23:4. Huo ungekuwa mwisho wa kesi ya Yesu, lakini Wayahudi walisisitiza kwamba alikuwa analipindua taifa. Wivu ndio uliowafanya makuhani wakuu wamshtaki Yesu, na Pilato alijua hivyo. Pia, alijua kwamba kumwachilia Yesu kungeleta shida, na alitaka kuepuka jambo hilo. Tayari kulikuwa na matatizo mengi, kwa kuwa Baraba na wengine walikuwa kifungoni kwa shtaka la uchochezi na mauaji. (Marko 15:7, 10; Luka 23:2) Isitoshe, mizozo iliyokuwa imetokea kati ya Pilato na Wayahudi ilikuwa imemharibia sifa mbele ya Tiberio aliyejulikana kwa kuwachukulia hatua kali magavana wabaya. Hata hivyo, kukubaliana na Wayahudi kungeonyesha udhaifu. Hivyo, Pilato hakujua la kufanya. Baada ya kujua Yesu alitoka eneo gani, Pilato alijaribu kutuma kesi hiyo kwa Herode Antipa, mtawala wa wilaya ya Galilaya. Hilo lilipokosa kufaulu, Pilato alijaribu kuwashawishi watu waliokusanyika nje ya nyumba yake waombe Yesu aachiliwe kulingana na desturi yake ya kumfungulia mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Umati ulipaaza sauti ukimtaka Baraba.—Luka 23:5-19. Huenda Pilato alitaka kufanya lililo sawa, lakini alitaka pia kutetea cheo chake na kuupendeza umati. Mwishowe, badala ya kusikiliza dhamiri yake na kufuatia haki, alitanguliza kazi yake. Aliomba maji, akanawa mikono na kudai kwamba hakuwa na hatia kwa kifo ambacho aliamuru.* Ingawa alijua kwamba Yesu hakuwa na hatia, Pilato aliagiza apigwe mijeledi na kuwaruhusu askari-jeshi wamdhihaki, wampige, na kumtemea mate.—Mathayo 27:24-31. Pilato alijaribu kwa mara ya mwisho kumwachilia Yesu, lakini watu wakapaaza sauti kwamba akimfungua, yeye si rafiki ya Kaisari. (Yohana 19:12) Pilato aliposikia hivyo, alifanya walivyotaka. Msomi mmoja alisema hivi kuhusu uamuzi wa Pilato: “Suluhisho ni rahisi: muue mtu huyo. Kinachopotea tu ni uhai wa Myahudi mmoja ambaye anaonekana kuwa hana maana yoyote; ungekuwa upumbavu kusababisha ghasia kwa sababu yake.” Ni Nini Kilichompata Pilato? Tukio la mwisho lililorekodiwa kuhusu maisha ya Pilato lilihusu mapambano. Yosefo anasema kwamba Wasamaria wengi wenye silaha walikusanyika kwenye Mlima Gerizimu wakitaka kufukua hazina ambazo walidhani zilizikwa huko na Musa. Pilato aliingilia kati, na majeshi yake yakawaua watu kadhaa. Wasamaria walipeleka malalamiko yao kwa Lusio Vitelio, gavana wa Siria aliyekuwa na cheo cha juu kuliko Pilato. Hatujui iwapo Vitelio aliona kwamba Pilato alikuwa amepita mipaka. Hata hivyo, alimwamuru Pilato aende Roma kujibu mashtaka hayo mbele ya maliki. Lakini kabla ya kufika huko, Tiberio akafa. “Baada ya hapo, Pilato hatajwi tena katika historia ila katika hekaya mbalimbali,” lasema gazeti moja. Lakini watu kadhaa wamejaribu kueleza zaidi. Imedaiwa kwamba Pilato alibadilika akawa Mkristo. “Wakristo” wa Ethiopia wanamwona kuwa “mtakatifu.” Eusebio, aliyeandika mwishoni mwa karne ya tatu na mwanzoni mwa karne ya nne, alikuwa wa kwanza kati ya wengi kusema kwamba Pilato alijiua kama Yuda Iskariote. Hata hivyo, hakuna anayejua kwa hakika kilichompata Pilato. Yaelekea Pilato alikuwa mkaidi, asiyejali, na mkandamizaji. Hata hivyo, tofauti na maliwali wengi wa Yudea ambao walikuwa na cheo hicho kwa muda mfupi, Pilato alikuwa gavana kwa miaka kumi. Kwa maoni ya Waroma, Pilato alikuwa gavana hodari. Ametajwa kuwa mtu mwoga ambaye alikuwa na hatia ya kuruhusu Yesu ateswe na kuuawa ili ajifaidi. Wengine wanasema kwamba kazi ya Pilato haikuwa kutetea haki bali ilikuwa kudumisha amani na hali njema ya Waroma. Siku za Pilato zilikuwa tofauti sana na zetu. Hata hivyo, hakuna hakimu anayefuata haki anayeweza kumhukumu mtu ikiwa anamwona kuwa hana hatia. Kama Pontio Pilato hangekutana na Yesu, jina lake halingekuwa maarufu sana. C n P By Jumong S Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Likes:Sakasaka Mao, kilwakivinje, Lukataluko and 2 others Mega Mind Nyerere JF-Expert Member Yesterday at 6:34 AM #2 Kumbe huyo kwenye picha ndiye Pilato. Mbona hata hatishi Like Quote Reply Report Likes:mtu chake, The Icebreaker, Eminem jr and 2 others MLALE Senior Member Yesterday at 6:39 AM #3 Poncio Pilato Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Ras Jeff Kapita JF-Expert Member Yesterday at 6:44 AM #4 Safi sana mkuu tunashukuru kwa kutuwekea strue story mahususi ya mtu huyu Like Quote Reply Report Likes:Eminem jr MarkHilary JF-Expert Member Yesterday at 6:46 AM #5 Huyu jamaa alikua na hekima Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Likes:Eminem jr Jumong S JF-Expert Member Yesterday at 6:46 AM #6 ras jeff kapita said: Safi sana mkuu tunashukuru kwa kutuwekea strue story mahususi ya mtu huyu Pamoja sana rafiki. Warumi walikuwa vzr kimfumo wa serikali. Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Likes:ras jeff kapita Baba_Enock JF-Expert Member Yesterday at 6:47 AM #7 Pirato??? GPA ya 32 Like Quote Reply Report Likes:The Icebreaker K Kibuyu180 JF-Expert Member Yesterday at 7:02 AM #8 Safi na Hongera mkuu Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Monde Arabe JF-Expert Member Yesterday at 7:04 AM #9 Safi sana! Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Da'Vinci JF-Expert Member Yesterday at 7:05 AM #10 Hingera kwa mada nzurii Like Quote Reply Report Likes:Eminem jr U Undertwentyboy JF-Expert Member Yesterday at 7:30 AM #11 nilianza kukuelewa ila nivoiona picha ya pilato nimekua na mashaka kuwa unatulisha matango pori ya misri pilato na camera wapi na wapi mkuu Like Quote Reply Report Likes:jogi, dolevaby and mtu chake Eminem Jr JF-Expert Member Yesterday at 7:37 AM #12 Asante kwa kutuelewesha maana jamaa tulikuwa tunamuelewa juu juu tu Like Quote Reply Report E Edson Silumbe Member Yesterday at 7:47 AM #13 Simulizi nzuri Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Kelao JF-Expert Member Yesterday at 7:50 AM #14 Story ya kweli ila picha sio Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Likes:dolevaby and mtu chake Elli JF-Expert Member Yesterday at 7:52 AM #15 Asante sana Mpwa, sasa nitakua napata picha ya Mhusika "Akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, siku ya tatu akafufuka kutoka kwa Wafu, akapaa mbinguni..." Like Quote Reply Report Likes:Jumong S and mtu chake Wilbald JF-Expert Member Yesterday at 7:54 AM #16 Haliitwi bamba la kuvalia kifuani...inaitwa dirii Like Quote Reply Report Likes:jogi and Nuhu39 Mtu Chake JF-Expert Member Yesterday at 7:56 AM #17 Ndio huyo ktk picha? Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report Mtemi Mpambalioto JF-Expert Member Yesterday at 8:07 AM #18 Mega Mind Nyerere said: Kumbe huyo kwenye picha ndiye Pilato. Mbona hata hatishi haha pilato kapiga picha HD! au zaman kulikuwa na mikamera ya hivo! Like Quote Reply Report Kisikiji JF-Expert Member Yesterday at 8:08 AM #19 Mkuu kwenye picha tutake radhi, isije kutuaminisha kama baadhi wanavyoamini ya Yesu na kuiabudu. Like Quote Reply Report Likes:Nuhu39 Nuhu39 JF-Expert Member Yesterday at 8:17 AM #20 Alikuwa na busara katika uongozi wake. Sent using Jamii Forums mobile app Like Quote Reply Report 1 2 Next Share: Facebook Twitter Google+ Reddit WhatsApp Email Link Telegram Instagram Remove formatting Bold Italic Underline Text color Font size Insert link Insert image Smilies Insert Alignment List Undo Redo Toggle BB code Write your reply... POST REPLY PREVIEW ATTACH FILES Edit avatar sumbi fabian New Member Messages 3 Likes 0 Trophy points 3 FORUM STATISTICS THREADS 1,192,801 MEMBERS 452,071 POSTS 27,746,863 FACEBOOK TWITTER TELEGRAM INSTAGRAM Habari na Hoja mchanganyiko Previous WHO WE ARE JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic. You are always welcome! Read more... WHERE ARE WE? We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually. For anything related to this site please Contact us. Contact us now... DISCLAIMER JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users.. Read more... FORUM RULES JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you. You MUST read them and comply accordingly. Read more... PRIVACY POLICY We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one. Read our Privacy Policy. Proceed here... Next Contact usTerms and rulesJamiiForums' Privacy PolicyHelp Up to top

Saturday, August 11, 2018

KITU CHA KWANZA ALICHOKISEMA RICH MAVOKO BAADA YA KUSHINDA KESI DHIDI YA WBC

Baada ya kushinda kesi dhidi ya uongozi aliokuwa nao kwanza wa WCB ambapo kesi hiyo ilienda kusikilizwa katika ofizi za BASATA  nakuoneka kuwa Rich mavoko alisainishwa mkataba ulikuwa ukimkandamiza yeye pamoja na muziki wke kwa mara ya kwanza msnii huyo ametoa ujumbe mzito alkini wa kuishukuru BASATA kwa kumsaidia kutoka huko. Katika ukurasa wake wa instagram, Rich mavoko aliandika “Nimejifunza vingi lakini kikubwa ni umhimu wa kukaa karibu na walezi wetu maana changamoto ni nyingi, na kuna mengi lakini yote mnaweza kuyajua kama tukiwa karibu na nyie, leo mmenipa maana ya neno mama ni mama hata kama akiwa kilema, hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu.” Tangu kumekuwa na tetesi za Rich Mavoko kutoka katika lebel hiyo hakuwahi kuzungumza kitu chochote mpaka hapo alipomaliza kesi  hiyo na kuanza kuonekana kwa habari hiyo katika vyombo vya habari.

Friday, August 10, 2018

MAHAKAMA YAAMURU KUONDOLEWA ZACHARIA NA LAUWO KATIKA KESI INAYOMKABIRI ALIYEKUWA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA SC

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu au kuifuta kesi hiyo. Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hans Poppe na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo. Akitoa uamuzi huo leo mahakamani hapo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema bado wanaifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu lakini itafika mahali uvumilivu utawashinda na kama jamhuri wameshindwa basi waifute. Mahakama imeamuru Zacharia Hans Poppe (kulia) aondolewe kwenye kesi ya viongozi wa Simba SC “Ukiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” amesema Hakimu Simba. Awali, Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa, kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na tayari wameshaifanyia marekebisho hati ya mashtaka na kwamba wanasubiri kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kesi hiyo iendelee kwa mujibu wa sheria. Baada ya Wakili huyo kudai hayo, Aveva aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibu za kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa imechukua muda mrefu huku Wakili wa Jamhuri Shadrack Kimaro na Wakili Takukuru, wamekuwa wakirushiana mpira. Kwa upande wake Kaburu ambaye ni mshtakiwa wa pili amedai kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita wako mahabusu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo huku mawakili hao wakidai faili liko kwa DPP. Alidai mshtakiwa wa kwanza, Aveva ana matatizo ya kiafya na kwamba kila wiki anaenda kliniki kwa ajili ya matibabu hivyo basi kuendelea kurushiana mpira ni kuwaumiza na kwamba hadhani kama DPP ameshindwa kushughulikia kesi yao, bali ni ucheweshaji wa makusudi unaofanywa na mawakili hao katika kesi hiyo kutoka kwa DPP na Takukuru. Amedai upelelezi umeshakamilika kilichobaki ni kubadilisha hati hiyo ili kesi ianze kusikilizwa, hivyo basi anaiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibuni ili waweze kuwaona na kuwaonea huruma kuliko kupanga tarehe za mbali za wiki mbili. Wakili Swai alidai kuwa, hoja zilizotolewa na washtakiwa hao zina mashiko na kuahidi kushughulikia suala hilo. Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo had I Agosti 17 mwaka huu. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli. Wanadaiwa, kuwa  Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.

MATOKEO YA UPONYAJI UGONJWA WA UKIMWI

Mgonjwa aliyekuwa na virusi vya HIV atangazwa kutokuwa tena na virusi hivyo Watafiti nchini Uingereza wamebainisha kwamba raia mmoja wa taif...